Hamia kwenye habari

Kushoto kwenda kulia: Dada Nadezhda Korobochko, Ndugu Igor Kletkin, na Ndugu Nikolay Kononenko

APRILI 1, 2024
URUSI

“Sitavunja Utimilifu Wangu”

“Sitavunja Utimilifu Wangu”

Mahakama ya Jiji la Nikolaevsk-on-Amur iliyo katika Eneo la Khabarovsk itatangaza uamuzi wake hivi karibuni katika kesi inayowahusu Ndugu Igor Kletkin, Ndugu Nikolay Kononenko, na Dada Nadezhda Korobochko. Mwendesha-mashtaka bado hajatoa ombi la hukumu anayopendekeza.

Maelezo Mafupi Kuwahusu

Tunamshukuru Yehova kwa kuwatunza kwa upendo na na kuwategemeza wote wanaomtumaini na kutangaza: “Wewe ni Mungu wangu.”​—Zaburi 31:14.

Mfuatano wa Matukio

  1. Oktoba 11, 2021

    Nyumba ya Igor na ya Nadezhda zilifanyiwa msako. Igor aliwekwa kizuizini

  2. Oktoba 12, 2021

    Nadezhda alihojiwa

  3. Oktoba 13, 2021

    Igor aliachiliwa kutoka kizuizini

  4. Oktoba 14, 2021

    Igor na Nadezhda waliwekewa vizuizi vya kusafiri

  5. Septemba 27, 2022

    Nikolay aliwekewa vizuizi vya kusafiri

  6. Januari 16, 2023

    Kesi ya uhalifu ilianza