Hamia kwenye habari

Hamia kwenye yaliyomo

Je, Wajua?

Je, Wajua?

Je, ilikuwa sahihi kuwaita wanabiashara waliouza mifugo katika hekalu la Yerusalemu “wanyang’anyi”?

SIMULIZI la Injili ya Mathayo linasema hivi: “Yesu akaingia katika hekalu na kuwafukuza wale wote waliokuwa wakiuza na kununua katika hekalu, na kuzipindua meza za wale waliokuwa wakibadili pesa na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa. Naye akawaambia: ‘Imeandikwa, “Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,” lakini ninyi mnaifanya kuwa pango la wanyang’anyi.’”—Mt. 21:12, 13.

Rekodi za kihistoria za Wayahudi zinaonyesha kwamba wanabiashara wa hekaluni waliwapunja wateja wao kwa kuwatoza bei ghali sana. Kwa mfano, Mishna (Keritot 1:7) kinarekodi pindi fulani katika karne ya kwanza W.K. ambapo bei ya hua wawili hekaluni ilifikia dinari moja ya dhahabu. Bei hiyo ililingana na mshahara wa siku 25 wa mfanyakazi wa hali ya chini. Hua au njiwa walikuwa matoleo ambayo maskini walikubaliwa kuyatoa; hata hivyo, sasa ndege hao walikuwa wanauzwa kwa bei ghali sana. (Law. 1:14; 5:7; 12:6-8) Rabi Simeon ben Gamaliel alikasirishwa sana na hali hiyo hivi kwamba akapunguza idadi ya dhabihu zilizokuwa za lazima, hivyo, bei ya hua wawili ikapungua kabisa mara moja.

Kwa msingi huo, Yesu hakukosea alipowaita wanabiashara wa hekaluni “wanyang’anyi” kwa sababu ya pupa na kuwapunja watu.