Masomo Unayoweza Kujifunza Katika Biblia

Kitabu hiki kitakusaidia ujifunze historia, kuanzia simulizi la Biblia la uumbaji, kuzaliwa na huduma ya Yesu, hadi wakati wa kuja kwa Ufalme.

Barua Kutoka kwa Baraza Linaloongoza

Kitabu hiki kinaweza kutumiwaje?

Mungu Aliumba Mbingu na Dunia

Biblia inasema kwamba Mungu aliumba mbingu na dunia. Je, unamjua malaika aliyeumbwa kabla ya vitu vingine vyote?

Mungu Alimuumba Mwanamume na Mwanamke wa Kwanza

Mungu alimuumba mwanamume na mwanamke wa kwanza na kuwaweka katika bustani ya Edeni. Alitaka waanzishe familia na kuifanya dunia yote kuwa paradiso.

Adamu na Hawa Hawakumtii Mungu

Kwa nini mti mmoja ulikuwa wa pekee katika bustani ya Edeni? Kwa nini Hawa alikula tunda la mti huo?

Hasira Yasababisha Mauaji

Mungu alikubali dhabihu ya Abeli lakini aliikataa dhabihu ya Kaini. Kaini alipojua hilo alikasirika sana na akafanya jambo baya.

Safina ya Noa

Malaika walipokuja duniani na kujichukulia wanawake, walizaa watoto ambao walikuwa majitu. Jeuri ilienea kotekote. Lakini Noa alikuwa tofauti​—alimpenda na kumtii Mungu.

Watu Nane Waliokoka na Kuingia Katika Ulimwengu Mpya

Mvua ya Gharika ilinyesha kwa siku 40 mchana na usiku. Noa na familia yake walikaa ndani ya safina kwa zaidi ya mwaka mmoja. Hatimaye, Mungu aliwaambia watoke katika safina.

Mnara wa Babeli

Baadhi ya watu waliamua kujenga jiji na mnara ambao kilele chake kingefika mbinguni. Kwa nini Mungu alifanya wazungumze lugha tofauti-tofauti?

Abrahamu na Sara Walimtii Mungu

Kwa nini Abrahamu na Sara waliacha maisha yao mazuri na kuhamia nchi ya Kanaani?

Hatimaye Wapata Mtoto!

Mungu alitimizaje ahadi yake kwa Abrahamu? Ni mtoto yupi wa Abrahamu aliyehusika, Isaka au Ishmaeli?

Mkumbuke Mke wa Loti

Mungu alinyesha mvua ya moto na kiberiti katika majiji ya Sodoma na Gomora. Kwa nini majiji hayo yaliharibiwa? Kwa nini tunapaswa kumkumbuka mke wa Loti?

Jaribu la Imani

Mungu alimwambia Abrahamu hivi: ‘Tafadhali, mchukue mwana wako wa pekee na umtoe akiwa dhabihu kwenye mmoja kati ya milima ya Moria.’ Abrahamu alikabili jinsi gani jaribu hilo la imani?

Yakobo Alipewa Urithi

Isaka na Rebeka walikuwa na watoto wawili mapacha, Esau na Yakobo. Kwa kuwa Esau alikuwa mzaliwa wa kwanza, angepata urithi wa pekee. Kwa nini aliuza haki hiyo kwa bakuli la mchuzi?

Yakobo na Esau Wafanya Amani

Yakobo alipata jinsi gani baraka kutoka kwa malaika? Na alifanyaje amani na Esau?

Mtumwa Aliyemtii Mungu

Yosefu alifanya mambo mazuri, lakini bado aliteseka sana. Kwa nini?

Yehova Hakumsahau Yosefu Kamwe

Ingawa Yosefu alikuwa mbali na familia yao, Mungu alimthibitishia kwamba alikuwa pamoja naye.

Ayubu Alikuwa Nani?

Alimtii Yehova hata ilipokuwa vigumu.

Musa Aliamua Kumwabudu Yehova

Alipokuwa mtoto, Musa aliokolewa kwa sababu ya hekima ya mama yake.

Mti Unaowaka Moto

Kwa nini moto haukuuteketeza mti huo?

Mapigo Matatu ya Kwanza

Farao aliwasababishia watu wake msiba kwa sababu kiburi kilimzuia achukue hatua moja tu rahisi.

Mapigo Sita Yaliyofuata

Mapigo hayo yalitofautianaje na mapigo matatu ya kwanza?

Pigo la Kumi

Pigo la mwisho lilikuwa baya sana hivi kwamba hata Farao mwenye kiburi alikubali mwishowe kuwaruhusu Waisraeli waondoke.

Muujiza Katika Bahari Nyekundu

Farao aliokoka mapigo kumi, lakini je, aliokoka muujiza huu wa Mungu?

Waisraeli Wamtolea Yehova Ahadi

Waisraeli walimtolea Mungu ahadi ya pekee walipokuwa wamepiga kambi kwenye Mlima Sinai.

Walivunja Ahadi Yao

Musa alipokuwa akipewa zile Amri Kumi, watu walitenda dhambi nzito.

Maskani ya Ibada

Hema hilo la pekee lilikuwa na sanduku la agano.

Wale Wapelelezi Kumi na Wawili

Ripoti ya Yoshua na Kalebu ilikuwa tofauti na ya wale wapelelezi wengine kumi ambao waliipeleleza nchi ya Kanaani.

Walimwasi Yehova

Kora, Dathani, Abiramu, na wanaume wengine 250 walikosa kutambua jambo fulani muhimu kumhusu Yehova.

Punda wa Balaamu Azungumza

Punda aliona mtu ambaye Balaamu hangeweza kumwona.

Yehova Amchagua Yoshua

Mungu alimpa Yoshua maagizo yanayoweza kutusaidia leo vilevile.

Rahabu Awaficha Wapelelezi

Kuta za Yeriko zilianguka chini. Lakini nyumba ya Rahabu iliendelea kusimama, hata ingawa ilikuwa imejengwa kwenye ukuta.

Yoshua na Wagibeoni

Yoshua alisali kwa Mungu na kusema: “Jua, simama tuli!” Je, Mungu alijibu?

Kiongozi Mpya na Wanawake Wawili Jasiri

Baada ya Yoshua kufa, Waisraeli walianza kuabudu sanamu. Maisha yakawa magumu, lakini Yehova akawasaidia kupitia mwamuzi Baraka, nabii wa kike Debora, na Yaeli!

Ruthu na Naomi

Wanawake wawili ambao walifiwa na waume zao walirudi Israeli. Mmoja kati ya wanawake hao, Ruthu, alienda kufanya kazi mashambani, na huko Boazi akamwona.

Gideoni Aliwashinda Wamidiani

Baada ya Wamidiani kuwakandamiza Waisraeli kwa muda fulani, watu walianza kumwomba Yehova msaada. Jeshi dogo la Gideoni liliwezaje kuwashinda askari 135,000 Wamidiani?

Hana Alisali Apate Mtoto

Elkana, Hana, Penina, na watoto wao walienda kuabudu katika maskani huko Shilo. Wakiwa huko, Hana alisali ili apate mtoto. Mwaka uliofuata, Samweli akazaliwa!

Ahadi ya Yeftha

Yeftha alitoa ahadi gani, na kwa nini? Binti Yeftha alitendaje kuhusu ahadi ya baba yake?

Yehova Azungumza na Samweli

Kuhani Mkuu Eli alikuwa na watoto wawili waliotumikia wakiwa makuhani katika maskani, lakini hawakutii sheria za Yehova. Kijana Samweli alikuwa tofauti kabisa. Usiku mmoja Yehova alizungumza na Samweli.

Yehova Alimfanya Samsoni Awe na Nguvu

Mungu alimfanya Samsoni kuwa Mnadhiri na alimpatia nguvu nyingi sana. Delila alipomnyoa nywele zake, Wafilisti walimkamata.

Mfalme wa Kwanza wa Israeli

Ingawa Yehova alikuwa amewapa Waisraeli waamuzi wa kuwaongoza, walitaka wawe na mfalme. Samweli alimtia mafuta Sauli awe mfalme wa kwanza wa Israeli, lakini baadaye Yehova alimkataa Sauli. Kwa nini?

Daudi na Goliathi

Yehova anamchagua Daudi kuwa mfalme wa Israeli anayefuata, na Daudi anaonyesha kwa nini huo ulikuwa uchaguzi unaofaa.

Daudi na Sauli

Kwa nini mwanamume mmoja alimchukia mwenzake, na yule aliyechukiwa alitendaje?

Yonathani Alikuwa Jasiri na Mshikamanifu

Mwana wa mfalme alikuwa rafiki wa karibu wa Daudi.

Dhambi ya Mfalme Daudi

Uamuzi mbaya unaleta matatizo mengi sana.

Hekalu kwa Ajili ya Yehova

Mungu akubali ombi la Mfalme Sulemani na kumpa mapendeleo mengi.

Ufalme Wagawanyika

Waisraeli wengi waacha kumwabudu Yehova.

Jaribu Kwenye Mlima Karmeli

Mungu wa kweli ni nani? Yehova au Baali?

Yehova Amwimarisha Eliya

Je, unafikiri anaweza kukuimarisha pia?

Mwana wa Mjane Afanywa Kuwa Hai Tena

Miujiza miwili katika nyumba ileile!

Malkia Mwovu Aadhibiwa

Yezebeli anapanga njama ya kumwua Nabothi ili amnyang’anye shamba lake la mizabibu! Yehova Mungu anaona uovu na tendo lake la ukosefu wa haki.

Yehova Amlinda Yehoshafati

Mfalme Yehoshafati asali kwa Mungu Yuda inapotishwa na mataifa adui.

Shujaa na Msichana Mdogo

Msichana Mwisraeli alimweleza mke wa bwana mkubwa wake kuhusu nguvu za Yehova, naye Naamani akaponywa kimuujiza.

Jeshi la Yehova Lenye Farasi na Magari ya Vita ya Moto

Jinsi mtumishi wa Elisha alivyoona kwamba ‘kuna wengi walio pamoja nasi kuliko wale walio pamoja nao.’

Ujasiri wa Yehoyada

Kuhani mwaminifu anampinga kuhani mwovu.

Yehova Alimwonyesha Yona Subira

Ni jambo gani lililofanya nabii mmoja wa Mungu amezwe na samaki mkubwa? Alitokaje katika samaki huyo? Na Yehova alimfundisha jambo gani?

Malaika wa Yehova Alimlinda Hezekia

Maadui wa Yuda wanasema kwamba Yehova hatawalinda watu wake, lakini wamekosea!

Yosia Aliipenda Sheria ya Mungu

Yosia anaanza kutawala akiwa na umri wa miaka nane, naye anawasaidia watu wake kumwabudu Yehova.

Yehova Amtuma Yeremia Akahubiri

Mambo ambayo nabii huyu kijana alisema yaliwafanya wazee wa Yuda wakasirike sana.

Yerusalemu Laharibiwa

Watu wa Yuda waendelea kuabudu miungu ya uwongo, hivyo Yehova awaacha.

Wavulana Wanne Walimtii Yehova

Wavulana Wayudea waliazimia kubaki waaminifu kwa Yehova hata walipokuwa katika makao ya mfalme huko Babiloni.

Ufalme Ambao Utadumu Milele

Danieli aeleza maana ya ndoto ya ajabu ya Nebukadneza.

Hawakuinamia Sanamu

Shadraki, Meshaki, na Abednego wakataa kuabudu sanamu ya dhahabu ya mfalme wa Babiloni.

Ufalme Unaofananishwa na Mti Mkubwa

Ndoto ya Nebukadneza yatabiri wakati wake ujao.

Mwandiko Ukutani

Maandishi hayo ya ajabu yalitokea wakati gani, nayo yalimaanisha nini?

Danieli Ndani ya Shimo la Simba

Sali kwa Yehova kila siku, kama Danieli alivyofanya!

Esta Awaokoa Watu Wake

Ingawa alikuwa yatima kutoka nchi nyingine, baadaye alikuwa malkia.

Ezra Alifundisha Sheria ya Mungu

Baada ya Waisraeli kumsikiliza Ezra, walimtolea Mungu ahadi ya pekee.

Kuta za Yerusalemu

Nehemia alipogundua kwamba maadui wake walitaka kuwashambulia, kwa nini hakuogopa?

Elisabeti Apata Mtoto

Kwa nini mume wa Elisabeti aliambiwa kwamba hangeweza kuzungumza mpaka mtoto azaliwe?

Gabrieli Amtembelea Maria

Alimpa ujumbe uliobadili maisha yake.

Malaika Watangaza Kuzaliwa kwa Yesu

Wachungaji waliosikia tangazo hilo walichukua hatua haraka.

Yehova Alimlinda Yesu

Mfalme mwovu alitaka kumwua Yesu.

Yesu Akiwa Kijana

Ni kwa njia gani Yesu aliwashangaza walimu hekaluni?

Yohana Anatayarisha Njia

Yohana anakuwa nabii anapokuwa mtu mzima. Anafundisha kwamba Masihi anakuja. Watu wanaitikiaje ujumbe wake?

Yesu Anakuwa Masihi

Yohana anamaanisha nini anaposema kwamba Yesu ndiye Mwana-Kondoo wa Mungu?

Ibilisi Anamjaribu Yesu

Ibilisi anamjaribu Yesu mara tatu. Vishawishi hivyo vitatu ni nini? Yesu anatendaje?

Yesu Analisafisha Hekalu

Kwa nini Yesu anawafukuza wanyama nje ya hekalu na kupindua meza za wanaobadili pesa?

Mwanamke Kisimani

Mwanamke Msamaria anashangaa kamba Yesu anazungumza naye. Kwa nini? Yesu anamwambia jambo gani ambalo hakuwa amemwambia mtu mwingine yeyote?

Yesu Anahubiri Ujumbe wa Ufalme

Yesu anawaalika baadhi ya wanafunzi wake wawe ‘wavuvi wa watu.’ Baadaye, anawazoeza 70 kati ya wafuasi wake kuhubiri habari njema.

Yesu Anafanya Miujiza Mingi

Popote anapoenda, wagonjwa wanamfikia ili awasaidie, naye anawaponya wote. Hata anamfufua msichana mdogo.

Yesu Anachagua Mitume Kumi na Wawili

Kwa nini Yesu anawachagua? Je, unakumbuka majina yao?

Mahubiri ya Mlimani

Yesu aliufundisha umati uliokusanyika mambo muhimu sana.

Yesu Anawafundisha Wanafunzi Wake Jinsi ya Kusali

Yesu aliwaambia wanafunzi wake waendelee kuomba mambo gani?

Yesu Analisha Maelfu ya Watu

Muujiza huo unatufundisha nini kuhusu Yehova na Yesu?

Yesu Anatembea Juu ya Maji

Je, unaweza kuwazia jinsi ambavyo mitume walihisi walipoona muujiza huo?

Yesu Aponya Siku ya Sabato

Kwa nini si watu wote waliofurahishwa na mambo ambayo Yesu alifanya?

Yesu Amfufua Lazaro

Yesu alipomwona Maria akilia, yeye pia alianza kulia. Hata hivyo huzuni yao ikageuka na kuwa shangwe.

Mlo wa Mwisho wa Yesu

Yesu aliwapa mitume wake maagizo muhimu wakati wa mlo wao wa mwisho.

Yesu Akamatwa

Yuda Iskariote aliongoza umati wa watu wenye marungu na mapanga ili wamkate Yesu.

Petro Anamkana Yesu

Ni nini kilichotendeka katika ua wa nyumba ya Kayafa? Yesu alitendewa jinsi gani ndani ya nyumba?

Yesu Afa huko Golgotha

Kwa nini Pilato anaamuru Yesu auawe?

Yesu Afufuliwa

Ni mambo gani yenye kupendeza yanayotokea baada ya Yesu kuuawa?

Yesu Awatokea Wavuvi

Anafanya nini ili wamtambue?

Yesu Arudi Mbinguni

Lakini kabla ya kufanya hivyo, anawapa wanafunzi wake maagizo muhimu sana.

Wanafunzi Wapokea Roho Takatifu

Roho takatifu iliwapatia nguvu gani kimuujiza?

Hawakuvunjwa Moyo na Kitu Chochote

Viongozi wa kidini waliofanya Yesu auawe, wajaribu kuwanyamazisha wanafunzi. Lakini hawawezi.

Yesu Amchagua Sauli

Sauli ni adui mkatili wa Wakristo, lakini angebadilika baada ya muda mfupi.

Kornelio Apokea Roho Takatifu

Kwa nini Mungu alimtuma Petro nyumbani kwa mwanamume huyo, ambaye si Myahudi?

Ukristo Waenea Katika Mataifa Mengi

Mtume Paulo na waandamani wenzake wamishonari waanza kuhubiri katika maeneo ya mbali.

Mlinzi wa Jela Ajifunza Kweli

Hadithi hii inahusuje roho mwovu, tetemeko la nchi, na upanga?

Paulo na Timotheo

Wanaume hao wawili walifanya kazi pamoja wakiwa marafiki na wafanyakazi wenzi.

Paulo Apelekwa Roma

Safari imejaa hatari, lakini hakuna hali yoyote ngumu inayoweza kumzuia mtume huyu.

Ufunuo kwa Yohana

Yesu alimpa mfululizo wa maoni kuhusu wakati ujao.

“Ufalme Wako na Uje”

Ufunuo kwa Yohana unaonyesha jinsi Ufalme wa Mungu utakavyobadili maisha duniani.